• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yajiunga tena na Shirika la posta duniani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu

    (GMT+08:00) 2019-04-11 19:28:48

    Somalia imejiunga tena rasmi na shirika la posta duniani baada ya vikwazo vilivyokuwepo kwa zaidi ya miongo miwili kuondolewa.

    Waziri wa posta, mawasiliano ya simu na teknolojia Bw. Bishar Hussein, wiki hii wamesaini makubaliano ya mpango wa Somalia kulipa madeni yake ya muda wa miaka 10 kuanzia mwaka huu.

    Deni hilo ni pamoja na malimbikizo ya ada ya uanachama kutoka mwaka 1982 ambayo imefikia dola milioni 1.88 za kimarekani.

    Makubaliano hayo yana maana kuwa nchi zote wanachama wa Shirika la posta duniani, zitaanza tena kutuma barua nchini Somalia baada ya taratibu kukamilishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako