• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Diego Costa apewa adhabu kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi

  (GMT+08:00) 2019-04-12 07:56:31
  Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa amerudi tena kwenye vichwa vya habari vya wadau wa soka baada ya kukutana na adhabu ya kufungiwa kucheza mechi 8 za ligi kuu ya Uhispania maarufu kama La Liga baada ya kuthibitika kuwa mchezaji huyo alitumia lugha ya matusi kwa refa Jesus Gil katika mchezo baina ya timu yake na FC Barcelona.

  Costa alitumia lugha hiyo baada ya kutokubaliana na maamuzi ya mwamuzi huyo, akilalamika kuchezewa faulo ila kutokana na kutoa lugha chafu alijikuta akizawadiwa kadi nyekundu dakika ya 28 na kutolewa nje ya uwanja. Madrid ilipoteza mchezo huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako