• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa Sudan aapishwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito

    (GMT+08:00) 2019-04-12 08:44:07

    Waziri wa ulinzi wa Sudan Bw. Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf ameapishwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito la nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Sudan, Bw. Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf amekula kiapo kwa kufuata katiba ya nchi na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Kijeshi la Mpito, na Bw. Kamal Abdul-Marouf Al-Mahi kuwa naibu wake.

    Mapema Alhamisi, Bw. Ibn Auf alitangaza kuondolewa madarakani kwa rais Omar al-Bashir wa Sudan na serikali yake, pia alitangaza hali ya hatari ya taifa kwa miezi mitatu na marufuku ya kutoka nje wakati wa usiku kwa mwezi mmoja.

    Waziri huyo amesema baraza la kijeshi litaundwa kusimamia nchi katika kipindi cha mpito cha miaka miwili.

    Pia ametangaza kusitishwa kwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Sudan, na kufungwa kwa anga na vivuko vyote vya mpakani kwa saa 24 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako