• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaboresha mfumo wa huduma za afya ili kukabiliana na maradhi

    (GMT+08:00) 2019-04-12 09:09:21

    Mke wa rais wa Kenya bibi Margaret Kenyatta amesema serikali ya nchi hiyo inajitahidi kuufanyia mageuzi mfumo wa huduma za afya, ili kuongeza ubora na ustahimili wake wakati nchi hiyo inashuhudia kuongezeka kwa mzigo wa maradhi.

    Bibi Kenyatta amesema hayo jana alipohutubia mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya Mifumo Bora ya Afya ya Tume ya Kimataifa ya Afya ya Lancet. Amesema upatikanaji wa matibabu bora na ya gharama nafuu ni muhimu kwa kudhibiti vifo vinavyotokana na sababu zinazozuilika.

    Amesema ni lazima kuboresha mfumo wa afya kwa kuchukulia matibabu bora kuwa kiini cha mapambano dhidi ya maradhi.

    Ripoti ya Lancet inasisitiza kuwa matibabu bora ni mkakati mkubwa wa kuharakisha kutimizwa kwa malengo ya maendeleo yanayohusika na afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako