• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC yatoa wito wa misaada kwa watu walioathiriwa na kimbunga Idai

    (GMT+08:00) 2019-04-12 09:10:15

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC ambaye pia ni rais wa Namibia Bw. Hage Geingob ametaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo watoe misaada ya kibinadamu ili kukabiliana na maafa yaliyosababishwa na kimbunga Idai.

    Rais Geingob amesema kimbunga hicho kimesababisha uharibifu mkubwa wenye athari za kiuchumi na miundombinu kwa wakati huu, muda mfupi na kwa muda mrefu.

    Amesisitiza mahitaji ya juhudi za pamoja za ukanda huo, kwani rasilimali za nchi zilizoathiriwa na kimbunga hicho haziwezi kukabiliana na maafa hayo kwa pande zote.

    Kutokana na athari ya kimbunga Idai, karibu watu milioni tatu wanahitaji misaada ya kibinadamu ya haraka, ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, nguo, maji safi ya kunywa, afya na matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako