• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China na mwenzake wa Croatia wakagua kwa pamoja mradi wa daraja la Peljesac

    (GMT+08:00) 2019-04-12 10:18:11

    Waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic pamoja na mgeni wake waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang wamekagua mradi wa daraja la Peljesac linalojenga na kampuni ya China katika peninsula ya Peljesac, nchini Croatia.

    Bw. Plenkovic amesema, kampuni ya China imeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo kwa haki na usawa, na anaamini kuwa ujenzi wa daraja hilo lililosubiriwa kwa miaka mingi na watu wa Croatia utakamilika kama ilivyopangwa. Ameongeza kuwa daraja hilo si kama tu litarahisisha usafiri wa umma, na bali pia litatoa fursa kwa makampuni ya China kufungua soko jipya, na kutoa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa kiutendaji kati ya Ulaya na China.

    Baada ya kufahamishwa maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Bw. Li amesema, daraja hilo limeonesha urafiki na ushirikiano mzuri kati ya nchi hizo mbili. Amesisitiza kuwa, kampuni ya China inapaswa kutimiza malengo yote ya makubaliano na kutumia vifaa bora kujenga daraja kwa ubora wa juu.

    Habari zinasema, jumatano wiki hii, Bw. Li alishiriki kwenye mkutano wa 8 wa mawaziri mkuu wa China na nchi za Ulaya ya kati na mashariki uliofanyika mjini Dubrovnik na kukutana na mawaziri mkuu wa Slovakia, Albania, Jamhuri ya Czech, Slovenia, Serbia na Bulgaria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako