• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaodhaniwa wapiganaji wa Al Shabaab wawateka madaktari wawili wa Cuba kwenye mji wa mpakani wa Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-12 18:23:04
    Watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab wamewateka madaktari wawili kutoka Cuba kwenye shambulizi walilofanya barabarani, kwenye eneo la Mandera kaskazini mashariki mwa Kenya.

    Wana usalama na maofisa wa serikali ya huko, wamesema wapiganaji hao kwanza walilizuia gari lililokuwa limewabeba madaktari hao saa tatu asubuhi, kabla ya kumfyatulia risasi na kumuua polisi aliyekuwa anawalinda madaktari hao. Madaktari hao walikuwa wanakwenda kazini, na wapiganaji hao wanadhaniwa kuvuka mpaka kutoka Somalia. Operesheni kubwa imeanza ili kuwatafuta wahanga hao, na polisi wa Kenya wametangaza kuwa mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo amekamatwa. Mtuhumiwa huyo alikuwa ni dereva wa madaktari hao.

    Madaktari wapatao 100 kutoka Cuba wanafanya kazi katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ikiwa ni sehemu ya mpango wa makubaliano kati ya serikali za nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako