• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kusambaza miche 100000 ya minazi wakati ya mvua ya masika

    (GMT+08:00) 2019-04-12 19:19:49

    Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Tanzania imesema inakusudia kusambaza miche ya minazi 100,000 katika kipindi cha mvua za masika ili kuimarisha na kurudisha hadhi ya zao la nazi Zanzibar ambalo hivi sasa uzalishaji wake umepungua.

    Akizungumza na radio China Kimataifa, mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Mali nchini Tanzania Bw Soud Mohamed alisema zao la minazi limeshuka uzalishaji wake kwa sababu mbalimbali ikiwamo ukataji wa miti hiyo kwa ajili ya matumizi ya mbao na shughuli za ujenzi.

    Aidha, alisema miti hiyo inaendelea kupunguwa kwa kiwango kikubwa kutokana na kasi ya ujenzi katika maeneo ya vijijini ambapo mtu hulazimika kukata mnazi ili kupata nafasi ya kujenga.

    Alisema wizara inatarajiwa kusambaza miche ya mikarafuu milioni moja ili kuimarisha zao hilo.

    Mkuu wa vitalu vya Idara ya Kilimo, Khadija Mohamed Said, alisema tayari miche ipo na kwa sasa inasubiri kusambazwa kwa wakulima.

    Aliitaja baadhi ya miti ambayo pia itasambazwa kwa wakulima ni ya matunda kama miembe kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa matunda hayo.

    Alieleza kwamba miche hiyo inatarajiwa kusambazwa katika mashamba ya serikali pamoja na wananchi kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako