• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama vitatu vya Jua kali Kenya vyapewa tenda ya kutengeneza madirisha kwa mradi wa serikali

    (GMT+08:00) 2019-04-12 19:20:08

    Vyama vitatu vya wafanyakazi wa Jua kali nchini Kenya vimepatiwa kandarasi ya kutengeneza madirisha 8,400 na milango elfu 7 ya mradi wa nyumba za gharama nafuu katika eneo la Parklands mjini Nairobi.Katibu wa nyumba Bw Charles Hinga amesema vyama vya Ngong Road, Kariobangi na Kamukunji pia vimesaidiwa kupata mkopo wa shilingi milioni 200 ambao utawawezesha kutengeneza bidhaa hizo.

    Akizungumza mjini Nairobi, katibu Hinga amesema nyumba 300 za kwanza zitakuwa tayari ifikapo Septemba mwaka huu.Hii ni sehemu ya serikali ya kupiga jeki sekta ya jua kali nchini Kenya katika kufanikisha mradi wa nyumba za bei nafuu. Nyumba hizo 1,370 ambazo zinajengwa na kampuni ya ujenzi ya China zinajengwa kwenye kipande cha ardhi cha hekari 7-9. Aidha nyumba hizo zitauzwa kwa kati ya shilingi laki 6 hadi milioni 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako