• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaitaka TALIRI kufanya utafiti wa kitaifa kuondoa ya ulegevu katika uwajibikaji

    (GMT+08:00) 2019-04-12 19:20:27

    Serikali ya Tanzania imeitaka Bodi ya Taasisi ya Utafiti Mifugo Tanzania (TALIRI) kufanya utafiti wa kitaifa ili kuondoa dhana kwamba wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo ni taasisi za kimataifa.

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw Luhaga Mpina alisema bodi hiyo inatakiwa kwenda kufanya mabadiliko ili sekta ya mifugo ikue tofauti na ilivyo sasa.

    Alisema lengo ni kuzionyesha taasisi nyingine ambazo hazina mpango wa kufanya utafiti za ndani ya nchi.

    Waziri Mpina alisema lengo ni kuona wanakwenda vizuri ili kuiaminisha jamii kuwa wanaweza.

    Alisema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na mifugo mingi, lakini uzalishaji wa maziwa bado upo katika kiwango cha chini, jambo ambalo halileti picha nzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako