• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti mpya wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan aapishwa

    (GMT+08:00) 2019-04-13 18:38:45

    Bw. Abdel-Fattah al-Burhan Abdel-Rahman jana alikula kiapo kwa mujibu wa katiba na kuwa mwenyekiti mpya wa Baraza la Kijeshi la Mpito. Abdel-Rahman amechukua nafasi ya Bw. Awad Mohamed Ahmed Ibn Auf ambaye jana mapema alitangaza kujiuzulu. Juzi Alhamis Waziri wa ulinzi wa Sudan Ibn Auf alitangaza kumuondoa madarakani rais Omar al-Bashir na serikali yake. Amechukua nafasi ya uenyekiti wa baraza la kijeshi la mpito na kuongoza nchi kwa kipindi cha miaka miwili.

    Wakati huohuo Vikosi vya RSF jana vilitoa wito wa kuundwa kwa baraza la mpito la kijeshi na serikali ya kiraia katika kipindi cha mpito cha miezi mitatu hadi sita. Kwenye taarifa yake RSF imesema ni muhimu kufungua mlango kwaajili ya mazungumzo na sekta mbalimbali za kijamii na kuharakisha kupanga mikutano ya mazungumzo na viongozi wa vyama vya kisiasa, shirikisho la wataalamu wa Sudan na viongozi wa mashirika ya vijana na asasi za kiraia. Aidha imetaka kuwekwa mpango maalumu wa kipindi cha mpito cha miezi mitatu hadi sita na kurekebisha katiba kupitia kamati ya katiba inayohusisha nguvu zote za Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako