• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafikiria kuanzisha sera ya kuongeza kasi ya kuuza magari yake katika nchi za Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2019-04-13 18:54:55

    Kenya inapanga kuanzisha sera itakayoongeza kasi ya kuuza magari yake katika nchi za Afrika Mashariki.

    Akiongea na wanahabari mjini Nairobi katika semina ya kuthibitisha sera ya taifa ya magari, mkurugenzi wa maendeleo ya sekta binafsi katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano, Stephen Odua, amesema wadau wote husika hivi sasa wanapitia sera ya taifa ya magari. Ameongeza kuwa sera hiyo itakapokuwa tayari itaisaidia Kenya kuongeza uzalishaji wa ndani wa magari ili usafirishaji wa magari ya nchi hiyo katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uweze kuongezeka kutoka asilimia 5 ya hivi sasa hadi asilimia 15 ifikapo mwaka 2022.

    Odua amebainisha kuwa ukuaji wa sekta ya magari nchini ulipungua kasi kutokana na uchumi huria ulioruhusu kuingia magari ya bei rahisi ya mitumba, na kwamba asilimia 85 ya magari yote yanayosajiliwa kila mwaka yanatoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako