• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuishawishi jumuiya ya kimataifa kupiga marufuku biashara ya kuvuka mpaka ya bidhaa za wanyama pori

    (GMT+08:00) 2019-04-14 17:02:31

    Kenya inatarajia kuishawishi jumuiya ya kimataifa kupiga marufuku biashara ya bidhaa za wanyama pori kufuatia tishio la kutoweka linalozikabili spishi muhimu kama tembo na vifaru.

    Akiongea wakati wa maandamano ya tembo, vifaru na wanyama wengine walio hatarini ambayo yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 4,000 wakiwemo maafisa wa serikali na wahifadhi wa wanyama, waziri wa utalii na wanyama pori wa Kenya Najib Balala amesema anadhamiria kuongoza kampeni ya dunia ya kuunga mkono marufuku ya biashara ya kuvuka mipaka ya bidhaa za wanyamapori. Amesisitiza kuwa serikali haitafumbia macho katika kuunga mkono marufuku ya biashara ya pembe za ndovu na spishi nyingine za wanyama zilizoko hatarini duniani.

    Kenya ni miongoni mwa nchi 130 zinazofanya maandamano ya kukuza uelewa juu ya hatari inayowakabili wanyama pori ikiwemo ujangili hali mbaya ya hewa na binadamu kuvamia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako