• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya mpito ya kijeshi ya Sudan yatangaza kuondoa marufuku ya kutotembea usiku nchini kote

    (GMT+08:00) 2019-04-14 17:25:26

    Mwenyekiti wa tume ya mpito ya kijeshi ya Sudan Bw. Abdel-Fattah Al-Burhan jana alitangaza kuondoa marufuku ya kutotembea usiku nchini kote.

    Bw. Burhan alitoa taarifa ya kuondoa marufuku hiyo na kuwaachia huru mahabusu na wafungwa waliohukumiwa kutokana na sheria ya hali ya dharura wakati wa serikali ya rais wa zamani Omar al-Bashir. Pia alitangaza kuwa, atajadiliana na vyama vyote vya Sudan na kuunda serikali ya mpito itakayosimamia mambo ya taifa ndani ya muda wa mpito wa miaka miwili.

    Bw. Burhan alisisitiza kuwa atafanya juhudi kulinda usalama wa taifa, nakuwataka raia wa Sudan wafanye juhudi kwa pamoja ili kurudisha maisha ya kawaida.

    Aidha, jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imesema itaisaidia Sudan inayokabiliana na hali ya kuyumba kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako