• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mafuta wa Nigeria awaondoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa mafuta

    (GMT+08:00) 2019-04-15 09:02:24

    Waziri wa mafuta wa Nigeria Bw. Ibe Kachikwu amewaondoa hofu wananchi kutokana na uhaba wa mafuta unaozikumba baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

    Akiongea na wanahabari mjini Abuja, waziri huyo amesema nchi hiyo imepita kwenye kipindi cha uhaba wa mafuta na kuwataka wamiliki wa magari wasinunue mafuta kwa wingi kutokana na hofu.

    Bw. Kachikwu amewahakikishia wanigeria kuwa nchi hiyo ina mafuta ya kutosha. Kwa mujibu wa Kampuni ya mafuta ya taifa ya Nigeria NNPC, nchi hiyo ina akiba ya lita bilioni moja za mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako