• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yatoa mwito wa kubadilisha kwa mitaala ili kuinua mwamko kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-15 19:23:41

    Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira limetoa mwito wa kupitiwa upya kwa mitaala ya elimu barani Afrika, ili kuhimiza mwamko kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kwa vijana.

    Mratibu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika Bw. Richard Munang, amesema mjini Nairobi kuwa mitaala ya sasa haiwezi kutoa msukumo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa hiyo unahitaji kutoa ujuzi mpya unatakiwa kubadilisha changamoto kuwa fursa.

    Amesema mitaala ya sasa kwenye nchi nyingi za Afrika ina mifumo ya kikoloni, ambayo inatoa mkazo kwenye kujenga raslimali ya nguvu kazi kwa ajili ya maslahi ya nchi za kigeni, na sio kuhimiza maendeleo ya Afrika.

    Ametoa mfano kuwa Tehama inaweza kutoka mchango mkubwa kwenye kuhimiza mageuzi kwenye hatua zinazochukuliwa kwa ajili ya watu na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako