• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasema msukosuko wa kisiasa nchini Sudan haujaathiri usafirishaji wa mafuta

    (GMT+08:00) 2019-04-15 19:24:00

    Waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Bw. Ezekiel Lol Gatkuoth amesema usafirishaji wa mafuta kutoka kwenye maeneo yake ya kaskazini kuelekea kwenye bandari ya Port Sudan, haujaathiriwa na msukosuko wa kisiasa uliotokea nchini Sudan, baada ya jeshi la nchi hiyo kumwondoa madarakani Rais Omar al-Bashir.

    Bw. Gatkuoth amesema timu za kiufundi za pande mbili zinashirikiana vizuri na hakuna la kutia wasiwasi. Sudan Kusini inategemea miundombinu ya Sudan kusafirisha mafuta kutoka kwenye visima vyake.

    Habari nyingine zinasema msemaji wa baraza la mpito la kijeshi amesema kamati maalum imeundwa ili kupokea makao makuu ya Chama cha NPC na mali zake, na kusema chama hicho hakitakuwa na nafasi kwenye serikali ya kiraia. Msemaji huo pia amesema serikali itaendelea kuwakamata watu wote waliohusika na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako