Alisema kuna tatizo kubwa la takwimu za wakulima na kwamba kutokana na hali hiyo, wizara imeanza kuwasajili ili mazao wanayolima yatambulike, kwa ukubwa gani na wapo kwenye maeneo gani.
Alitaja mazao hayo kuwa ni pamba, miwa, korosho, kahawa, chai, pareto, alizeti na michikichi na hadi Machi 31, mwaka huu, wameshaandikishwa wakulima 1,274,337 sawa na asilimia 72.
Alisema lengo ni kuwafikia wakulima milioni 1.7 na kuzitaka bodi za mazao hayo zikamilishe kazidata hiyo ili kujua wako wapi.
Hasunga alisema kwa sasa kuna mashamba 134 makubwa ya kahawa, pareto, mkonge, chai, pamba na korosho na alitaka kujua kama kuna mazao mengine ambayo yana mashamba makubwa, hivyo akahimiza kukamilisha usajili ili kujua mashamba hayo.
Alilishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), kwa kutoa vifaa hivyo kwa ajili ya kusaidia usajili wa wakulima nchini humo kitengo ambacho kitaongeza ubora na uhakika wakulima walipo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |