• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama ya umeme kushuka Novemba kama makubaliano ya kuteremsha bei na Uganda yatafaulu

    (GMT+08:00) 2019-04-15 20:18:27

    Matumaini ya gharama ya umeme kwenda chini huenda yakatimia mwezi wa Novemba wakati Kenya itafanya mazungumzo kuhusu kununua umeme kutoka nchini Uganda. Wizara ya Nishati ya Kenya pia imewatia mikononi baadhi ya wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika nishati ya bei nafuu. Baadhi ya wawekezaji wamenunua mitambo kwa ajili ya shughuli hiyo.Waziri wa Nishati wa Kenya Bw Charles Keter amesema makubaliano hayo ya bei ya umeme kati ya Kenya na Uganda yaliyotiwa saini mwaka wa 2014 yataangaliwa upya ambapo bei itashuka na hatimaye wakenya kupunguziwa gharama ya umeme majumbani mwao.Hivi sasa Kenya inanunua Kilowati kwa saa moja shilingi 22 na bei hiyo inatarajiwa kupungua hadi shilingi 14 pindi pande zote mbili zitakapokubaliana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako