Wasagaji wa Nafaka nchini Kenya wamepinga madai ya serikali kuwa kuna magunia milioni 21 ya mahindi nchini Kenya. Kauli hiyo ya wasagaji unga inakuja wakati ambapo inadaiwa sababu ya kupanda kwa bei ya unga wa mahindi hadi shilingi 119 inatokana na kupungua kwa bidhaa hiyo.
Awali waziri wa kilimo alikuwa amesema kuna mahindi ya kutosha haoni haja ya wasagaji unga kuongeza bei ya unga wa mahindi.Wasagaji hao wa unga wamesema imewalazimu kuwaongezea wakulima wa mahindi shilingi elfu moja juu ya bei yao na serikali ili kuwatia moyo na kupokea mahindi hayo kwa wakati. Of the reported 21 million bags of maize available in the country, it was estimated that stocks held at household level are 13 million bags, representing 61 percent of the total produce. Ripoti inasema zaidi ya magunia ya mahindi milioni 13 yanazuiliwa na wakulima kutokana na bei mbaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |