• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yathibitisha mlipuko wa homa ya Crimea-Kongo katikati mwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-04-16 08:36:07

    Wizara ya afya ya Uganda imethibitisha mlipuko wa homa ya Crimea-Kongo CCHF katika eneo la Wakiso, katikati mwa nchi hiyo.

    Ofisa mwandamizi wa mawasiliano katika Wizara ya afya Bw. Emma Ainebyoona amesema, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 32 ambaye alifariki wiki iliyopita katika Hospitali kuu ya Entebbe amethibitishwa kuwa na maambukizi ya homa hiyo, na wanafamilia wake pamoja na wale walioshiriki kwenye mazishi yake, wanafuatiliwa na maofisa wa afya.

    Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, mlipuko wa homa ya Crimea-Kongo unatoa tishio kwa afya ya umma, na wastani wa asilimia 10 hadi 40 ya wagonjwa wa homa hiyo wanafariki dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako