• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yatafuta kibali cha Benki ya Dunia kwa utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija ya ardhi

    (GMT+08:00) 2019-04-16 08:36:27

    Serikali ya Zambia imetoa wito kwa Benki ya Dunia kuidhinisha utekelezaji wa mradi unaolenga kuimarisha ustahimili wa mfumo wa ikolojia na kuongeza tija ya ardhi kwenye sehemu ya kaskazini mwa nchi hiyo.

    Waziri wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa Bw. Alexander Chiteme amesema, Benki ya Dunia inapaswa kuidhinisha utekelezaji wa mradi wa Kuboresha Mazingira kwa ajili ya Maendeleo ya Ustahimilivu katika mikoa mitatu iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo.

    Amesema hayo alipokutana na mkurugenzi mwandamizi wa Mazingira na Utendaji Duniani wa Benki hiyo, Karin Erika Kemper, na mratibu wa nchi wa Benki ya Dunia Kusini mwa Afrika Benoti Bosquet na wakurugenzi wengine, kando ya Mikutano wa majira ya Spring ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia inayofanyika Washington.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako