• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 14 wauawa kwenye mapigano yaliyotokea kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani Darfur

    (GMT+08:00) 2019-04-16 08:58:54

    Shirika la habari la Sudan SUNA jana limesema, zaidi ya watu 14 wameuawa katika mapigano yaliyotokea kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani iliyoko jimboni Darfur, kusini mwa Sudan.

    Kaimu gavana wa Darfur Kusini Bw. Hashim Khalid amesema, mapigano hayo yalitokea Jumamosi kwenye kambi ya Kalma. Amesema silaha zimezagaa kwenye kambi hiyo ambayo imekuwa na hali mbaya ya kiusalama kutokana na kuwepo kwa wafuasi wa kundi la harakati za ukombozi wa Sudan, ambalo ni kundi kuu la waasi kwenye jimbo la Darfur.

    Vilevile ameongeza kuwa, serikali ya jimbo hairuhusiwi kuingia kwenye kambi hiyo inayoendeshwa na Tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako