• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanadiplomasia wa Sudan Kusini apongeza mtindo wa China katika kupambana na umaskini

    (GMT+08:00) 2019-04-16 10:02:03

    Balozi wa Sudan Kusini nchini China John Andruga Duku amepongeza mbinu inayotumia China katika kuondoa umaskini, ambayo imeifanya China iwe nchi kubwa ya pili kiuchumi duniani. Amesema mtindo wa kipekee wa maendeleo ya kiuchumi wa China umetoa mafunzo ya kutekelezeka kwa nchi yake inayojikwamua baada ya miaka mitano ya vita ya ndani. Ameongeza kuwa kilichoisaidia China kuondoa umaskini kwa kasi katika miaka 40 iliyopita ni maendeleo ya miundombinu na Sudan Kusini imepata maendeleo katika miundombinu kutokana na juhudi za kampuni za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako