• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan atumai uhusiano kati ya China na Sudan utafikia ngazi ya juu zaidi

    (GMT+08:00) 2019-04-16 10:22:25

    Balozi wa China nchini Sudan Bw. Ma Xinmin amekutana na mwenyekiti wa Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan Luteni Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan.

    Kwenye mazungumzo hayo, Luteni Jenerali Fattah al-Burhan amesema anatumaini kuwa uhusiano kati ya pande hizo mbili utafikia ngazi ya juu zaidi. Pia ameahidi kulinda kwa pande zote usalama na maslahi ya raia na makampuni ya China nchini humo.

    Balozi Ma Xinmin amesema, China inapenda kufanya juhudi kwa ajili ya kulinda na kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili. Pia inatetea kuwa nchi na mashirika yote ya kimataifa zinapaswa kuheshimu mamlaka ya Sudan na uhuru wake wa kisiasa, na kutoingilia kati mambo ya ndani ya Sudan. Ameongeza kuwa China inaamini kuwa Sudan ina uwezo na nguvu ya kushughulikia mambo ya ndani, na kulinda usalama na utulivu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako