• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni zinazomilikiwa na serikali kuu ya China zaendelea vizuri katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-04-16 16:52:38

    Msemaji wa kamati ya usimamizi na uendeshaji wa mali za taifa iliyo chini ya Baraza la Serikali ya China Bw. Peng Huagang leo amesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kampuni zinazomilikiwa na serikali kuu zimepata maendeleo mazuri, huku mageuzi ya sera ya umiliki wa kampuni hizo yakipiga hatua nzuri.

    Takwimu zilizotolewa leo na kamati hiyo zinaonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kampuni zinazomilikiwa na serikali kuu ya China zimedumisha maendeleo mazuri, na mchango uliotolewa na kampuni hizo kwa maendeleo ya uchumi na jamii pia umeendelea kuongezeka. Msemaji wa kamati hiyo Bw. Peng Huagang anasema,

    "Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, mapato ya kampuni za serikali kuu yalifikia dola za kimarekani zaidi ya trilioni moja, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.3 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Wakati huohuo mchango uliotolewa na kampuni hizo kwa maendeleo ya uchumi na jamii pia umeendelea kuongezeka, na kodi zilizotolewa na kampuni hizo zilifikia karibu dola bilioni 96.8 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 9.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu".

    Bw. Peng amesema hali nzuri ya maendeleo ya kampuni za serikali kuu inatokana na China kuendelea kukuza mageuzi, kuboresha mazingira ya biashara, na nguvu kubwa isiyoonekana ya maendeleo ya uchumi.

    Mwaka huu, ufanisi wa mageuzi ya kampuni za serikali kuu pia umedhihirika, na asilimia 70 ya kampuni zinazosimamiwa na kamati ya usimamizi na uendeshaji wa mali za taifa iliyo chini ya Baraza la Serikali ya China zimemaliza mageuzi ya sera ya umiliki. Bw. Peng anasema,

    "Katika mchakato wa mageuzi haya, tunahimiza mitaji ya kitaifa kuwekeza katika kampuni, na kujenga kampuni za vielelezo zenye kiwango cha juu zaidi duniani. Pia tunasukuma mbele mageuzi ya sera ya umiliki katika kampuni mia moja zinazomilikiwa na serikali kuu, na kampuni nyingine mia moja zinazomilikiwa na serikali za mitaa."

    Bw. Peng amesema kuhimiza mitaji ya kitaifa kufanya majaribio ya kuwekeza katika kampuni ni hatua muhimu ya mageuzi ya kampuni za serikali, na hadi sasa kampuni hizo za majaribio zimefikia 21. Ameongeza kuwa, China itaongeza nguvu katika kukabidhi madaraka, kurekebisha muundo na kufanyia mageuzi kampuni za serikali kwa kulingana na masoko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako