• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jengo la bunge la Zimbabwe lililojengwa kwa msaada wa China lahimiza ajira na maendeleo ya soko la ujenzi nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-04-16 18:55:44

    Ujenzi wa jengo jipya la bunge la Zimbabwe umeingia katika kipindi cha ujenzi wa msingi, wakati utekelezaji wa mradi huo umehimiza ajira na maendeleo ya soko la ujenzi nchini humo.

    Mkurugenzi wa mradi huo wa Kampuni ya Ujenzi ya Shanghai Bw. Cai Libo, amesema mradi huo umeajiri wenyeji zaidi ya 300, ambao wamepewa mafunzo na wafanyakazi wa China. Amesema wafanyakazi walioandaliwa katika mradi huo, wanakaribishwa sana katika sekta ya ujenzi ya huko, na uenezi wa vigezo vya China pia umehimiza maendeleo ya soko la ujenzi nchini humo.

    Ujenzi wa jengo jipya la bunge la Zimbabwe ni mradi mkubwa unaojengwa kwa msaada wa China katika eneo la kusini mwa Afrika, pia ni hatua muhimu ya kutekeleza ushirikiano kati ya China na Afrika. Mradi huo utakamilika mwezi Machi mwaka 2021.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako