• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UGANDA: MAUZO YA SIMITI NJE YAPANDA KWA ASILIMIA 25.

    (GMT+08:00) 2019-04-16 19:04:00
    Taifa la Uganda linajivuni kuendelea kuimarika kwa uuzaji wa simiti katika mataifa ya nje. Kulingana na ripoti iliyotolewa na benki ya Uganda, kumekuwa na ongezeko la mauzo kwa asilimia 24 mwaka wa 2018. Taifa la Uganda liliuza tani 393,952 za simiti ambazo thamani yake ni dola milioni 56, mwaka uliopita. Mauzo hayo ya mwaka uliopita, yalikuwa juu zaidi ya yale ya mwaka wa 2017, ambapo tani 295,726 ziliuzwa nje ya taifa. Thamani yake ilikuwa dola milioni 41.6. Katika ukanda huu wa Afrika, Uganda inachangia asilimia 30 ya simiti kwa mataifa ya nje. Inafuatwa na taifa la Rwanda kwa silimia 22 na nyingine ikichukuliwa na DR Congo na Sudan Kusini. Uzalishaji wa saruji nchini Uganda unataraijwa kuongezeka hadi kufikia tani milioni saba kwa mwaka. Nchini Kenya, uzalishaji wa saruji mwkaa jana, ulipungua kwa asilimia 8.5, hadi asilimia 5.64.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako