• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji kumaliza tathmini ya uharibifu uliosababishwa na kimbunga Idai

    (GMT+08:00) 2019-04-17 08:36:07

    Waziri wa kazi, makazi na rasilimali ya maji nchini Msumbiji Bw. Osvaldo Machatine amesema, tathmini ya uharibifu uliosababishwa na kimbunga Idai itakamilika katika wiki tatu.

    Akizungumza wakati wa semina ya tathmini ya mambo yanayohitajiwa baada ya majanga (PDNA), Bw. Machatine amesema ni mapema sana kuanza kutoa makadirio, lakini lengo la serikali ya nchi hiyo ni kwa mchakato wa tathmini kuwa na msingi wa utaratibu unaokubalika na jamii ya kimataifa. Amesema kazi hiyo itachanganuliwa na kuthibitishwa na wadau ndani ya utaratibu wa PDNA.

    Wakati huohuo, serikali ya Msumbiji imesema kuwa itaandaa mkutano na wafadhili katika mji wa Beira mwishoni mwa mwezi ujao ili kujadili ukarabati baada ya janga la kimbunga Idai. Mkutano huo pia utakusanya uzoefu kutoka kwa washiriki wa kimataifa kuhusu ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na kimbunga hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako