• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yasema iko tayari kutoa hifadhi ya kisiasa kwa aliyekuwa rais wa Sudan

    (GMT+08:00) 2019-04-17 08:36:24

    Wizara ya mambo ya nje ya Uganda imesema nchi hiyo iko tayari kumpa hifadhi ya kisiasa aliyekuwa rais wa Sudan, Omar al-Bashir, kama akiomba.

    Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Nw. henry Okello Aryem ameiambia kamati ya bunge ya masuala ya kimataifa kuwa, rais huyo aliyeondolewa madarakani, ni mdhamini wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini. Amesema mamlaka nchini Uganda zinafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Sudan, ambako maandamano yameendelea baada ya jeshi kumwondoa al-Bashir madarakani wiki iliyopita.

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda na aliyekuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir ni wadhamini wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako