• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la kijeshi la Sudan lawafuta kazi waendesha mashtaka wakuu watatu

    (GMT+08:00) 2019-04-17 08:51:16

    Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limetangaza kuwafuta kazi waendesha mashtaka wakuu watatu.

    Mwenyekiti wa baraza hilo Luteni Jenerali Abdel-Fattah Al-Burhan jana alitangaza uamuzi wa kuwaondoa kwenye nyadhifa zao mwendesha mashtaka mkuu Bw. Omer Ahmed Mohamed Abdel-Salam, msaidizi wake wa kwanza Bw. Husham Osman Ibrahim na mkuu wa mashtaka ya umma Bw. Amer Ibrahim Majib.

    Baraza hilo limemteua Bw. Al-Waleed Sid-Ahmed Mahmoud kuwa mwendesha mashtaka mkuu mpya.

    Mabadiliko hayo kwenye mfumo wa mahakama yanalenga kutimiza moja ya matakwa ya waandamanaji wa Sudan ambao wameendelea na mgomo wa kuketi nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum, licha ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Omar al-Bashir Alhamisi iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako