• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yatarajia kuimarisha ushirikiano na washirika wake

    (GMT+08:00) 2019-04-17 08:51:48

    Serikali ya Zambia imesema inatarajia kuimarisha ushirikiano na washirika wake kufuatia mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia iliyofanyika hivi karibuni.

    Waziri wa fedha Bibi Margaret Mwanakatwe, ambaye aliitaja mikutano hiyo ya majira ya Spring kuwa ni ya mafanikio, amesema serikali ilifanya mikutano kadhaa katika ngazi za pande mbili na pande nyingi, ambayo itaimarisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na washirika wake.

    Bi. Mwanakatwe amesema, vikao vya wawekezaji wa sekta mbalimbali vilivyofanyika kando ya mikutano hiyo, vimetoa matumaini kwa ujumbe wake kuhusu uwekezaji halisi, haswa kwenye nyanja za maendeleo ya nishati, teknolojia, viwanda, kilimo, elimu na huduma za jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako