• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gharama ya maisha yapanda Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-17 18:35:33

    Kupanda kwa bei ya chakula na mafuta kunaonekana kuwapa mzigo wakenya wengi hasa wenye mapato ya chini ambao tayari wameshindwa kumudu gharama ya maisha. Gharama ya bidhaa za kimsingi kama vile unga wa mahindi, maziwa, tomato na viazi vimekuwa vikipanda huku wafanya biashara wa bidhaa hizo wakidai kupungua kufuatia ukame ambao unaendelea hivi sasa. Bei ya mafuta pia imeonekana kupanda kwa miezi miwili mfululizo. Bei ya unga wa mahindi ambao ni bidhaa muhimu kwa wakenya wengi imepanda kwa asilimia 40 ndani ya wiki mbili na kufikia shilingi 119 kwa pakiti ya kilo mbili. Wasagaji wa Unga wamesema hali hiyo imechangiwa na upungufu wa mahindi katika soko. Gunia la kilo 90 la mahindi limekuwa likiuzwa kwa shilingi 3,200 wiki iliyopita kutoka shilingi 2,000 hapo awali. Wasagaji hao wa Unga wamesema huenda bei hiyo ikaendelea kupanda kama serikali haitaingilia kati.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako