• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli awakuna wadau wa SAGCOT

    (GMT+08:00) 2019-04-17 18:35:52
    Wadau wa Kituo Cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), wamepongeza hotuba ya kizalendo ya Rais John Magufuli kuhusu uwekezaji na kuelezea kuwa dhamira hiyo itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. Akizindua Kiwanda kipya cha Kuchakata chai cha Kabambe kinachomilikiwa na Kampuni ya Unilever Tanzania, Magufuli amewaonya watendaji katika ngazi zote serikalini kuachana na urasimu usio wa msingi kwa kukwamisha uwekezaji. Kwa upande wake, mwenyekiti wa Wood Foundation, Sir Ian Wood, amesema kauli ya Rais Magufuli imeonyesha dhamira ya wazi kuwa anakerwa na watendaji wachache wanaokwamisha ukuaji na maendeleo ya sekta za viwanda na uwekezaji. Mbali ya kumpongeza Magufuli, Sir Wood alisema taasisi yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na SAGCOT kwani kuwepo kwake kumechangia kuleta mageuzi mengi katika sekta ya kilimo katika ukanda huo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako