• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima alizeti wafundwa kufikia soko la kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-04-17 18:36:31
    Wakulima wa zao la alizeti nchini Tanzania wameshauriwa kutumia mbinu za asili ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kufikia soko la kimataifa katika nchi za Ulaya na India. Ushauri huo ulitolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Happines Mgalula wakati wa ufuguzi wa warsha ya tathmini ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika mnyororo wa thamani wa zao la alizeti iliyofanyika chini ya shirika la maendeleo la Uholanzi SNV.

    Mgalula, amesema wakulima wa zao hilo wanashauriwa kuzalisha kwa kutumia mbinu za asili ili kuweza kukidhi vigezo vya soko la kimataifa katika nchi za Ulaya na India.

    Alizitaja mbinu hizo kuwa ni kutumia mbolea za asili katika kupanda na mbegu bora pamoja na kutumia viuatilifu vinavyoshauriwa na wataalamu wa kilimo kwa kila eneo husika.

    Alibainisha kuwa zao hilo limepewa kipaumbele kuzalishwa hapa nchini kutokana na umuhimu wa kuongeza mafuta ya kula ambapo linachangia asilimia 51 ya mafuta yote yanayozalishwa na asilimia 40 ya mafuta yote yanayotumiwa hapa.

    Aidha, alisema mahitaji ya mafuta ya kula kwa sasa hapa nchini yanakadiriwa kuwa kati mita za ujazo 300,000 hadi 400,000 na kutokana na ongezeko la idadi ya watu mahitaji haya yataendelea kuongezeka kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako