• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani azungumza na rais wa zamani wa nchi hiyo Jimmy Carter kuhusu China

    (GMT+08:00) 2019-04-17 19:18:11

    Aliyekuwa rais wa Marekani Bw. Jimmy Carter amesema, rais Donald Trump wa nchi hiyo aliongea naye kuhusu China kwa njia ya simu, akieleza wasiwasi wake mkubwa kwamba, China itaipita Marekani kimaendeleo. Carter alimjibu hana wasiwasi huo kama yeye, na kusema Marekani ni nchi inayopenda vita zaidi duniani, ambapo China haikutumia pesa zake kwa ajili ya vita, na hii ndiyo sababu ya China inaweza kuishinda Marekani.

    Wakati baadhi ya wanasiasa wa Marekani akiwemo waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo wanaipaka matope China, Bw. Carter ambaye alipokuwa rais wa Marekani, China na Marekani zilianzisha uhusiano wa kibalozi, ameonesha busara yake kubwa na kuwajibika na maslahi ya taifa lake. Hali hii imethibitisha kuwa viongozi wa zamani wa Marekani bado ni nguvu muhimu ya kushughulikia masuala ya uhusiano kati ya China na Marekani. Na hii ndiyo ni sababu ya rais Trump kumpingia simu Bw. Carter na kumweleza wasiwasi wake, ili kujadili njia sahihi ya kukabiliana na China.

    Hivi sasa pato la taifa la China kwa mwaka limezidi dola za kimarekani trilioni 13.4, na kushika nafasi ya pili duniani. Hivyo wasiwasi wa Marekani unaongezeka na kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa wenye uhasama na China, na kwa sababu hiyo, Marekani ilianzisha vita ya kibiashara na kujaribu kuipaka matope China.

    Lakini katika zaidi ya mwaka mmoja uliopita, vitendo vya Marekani dhidi ya China havikupata matokeo yaliyotarajiwa. Bw. Carter alitahadhrisha mara nyingi kwamba, China ni muhimu kwa ustawi wa Marekani, na kama Marekani ikishindwa kuishi vizuri pamoja na China, nchi hizo mbili zote zitapata hasara. Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani imepunguza makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi wa Marekani kwa asilimia 0.2, na kuongeza makadirio ya maendeleo ya uchumi wa China kwa asilimia 0.1.

    Swali ni kwamba, ni vipi Marekani itafanya ili "iwe na nguvu tena"? Bw. Carter ametoa pendekezo lake lenye busara ya kimkakati. Amesema Marekani haipaswi kutumia fedha nyingi katika vita, wala kujaribu kuzishinikiza nchi nyingine kufuata mawazo yake. Ameongeza kuwa kama Marekani ikitoa dola za kimarekani trilioni tatu kutoka bajeti ya kijeshi kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu, labda itabaki trilioni mbili, lakini wamarekani watakuwa na reli ya mwendo kasi, barabara nzuri na madaraja yasiyobomoka, na mfumo wao wa elimu pia utaboreshwa na kuwa mzuri kama ule wa Korea ya Kusini na Hongkong.

    Ni dhahiri kwamba, kuacha vitendo vya upande mmoja, umwamba, na mabavu, kuzingatia maslahi ya wananchi, na kujiongezea uwezo wa ushindani, ni njia sahihi ya kuifanya Marekani "iwe na nguvu tena".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako