• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ligi ya Mabingwa Ulaya- Yasiyotarajiwa yamewezekana kwenye ulimwengu wa soka

    (GMT+08:00) 2019-04-18 09:48:55

    Usiku wa jana ulikuwa wa kusisimua zaidi katika michezo miwili iliyopigwa ya ligi ya mabingwa Ulaya michezo ya robo fainali ya mwisho. Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur ndio ilikuwa bonge moja la mechi kutokana na mvuto na presha ya mchezo huo ulivyokuwa kwa pande zote mbili.

    Hadi dakika 90 za mchezo kukamilika, Man City walipata magoli 4-3 lakini jumla ya kuu ya magoli ni 4-4 kwakuwa Man City ameruhusu magoli mengi nyumbani. Kwa matokeo hayo yamefanya Tottenham kutinga nusu fainali na watakutana na Ajax wakati Liverpool wao wamewafungashia virago FC Porto kwa kuwapiga bao 4-1, lakini jumla kuu ni magoli 6-1, watakutana na Barcelona ya Hispania.

    Michezo ya nusu fainali itakuwa ya kufa na kupona kwani kila timu itataka kukata tiketi ya kuingia fainali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako