• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juhudi za pamoja zahimizwa kuimarisha amani na usalama katika mpaka kati ya Ethiopia na Kenya

    (GMT+08:00) 2019-04-18 10:05:55

    Mkutano wa kikanda kuhusu amani katika mpaka kati ya Ethiopia na Kenya umesisitiza haja ya kufanya juhudi za pamoja kuhakikisha amani ya kudumu inayowezesha utatuzi wa changamoto za umaskini na maendeleo zinazozikabili jamii zilizoko kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

    Shirika la Pendekezo la Amani na Maendeleo la Kuvuka Mpaka kati ya Ethiopia na Kenya limeandaa mkutano wa ngazi ya juu wa siku mbili ulioanza jana huko Addis Ababa, ili kutafuta njia za kuimarisha amani na usalama kwa jamii zinazoishi katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.

    Mkutano huo unaunga mkono mapendekezo mengine yanayolenga kutatua mapigano na kuhakikisha amani ya kudumu na ukuaji wa uchumi katika maeneo ya mpakani, hususan maeneo ya Moyale-Marsabit, Omo-Turkana na Mandera.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako