• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Akiba ya fedha za kigeni ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu yaongezeka

    (GMT+08:00) 2019-04-18 19:13:56

    Msemaji wa mamlaka ya kusimamia fedha za kigeni ya China Bibi Wang Chunying, leo amesema mitaji inayovuka mipaka inaendelezwa kwa njia madhubuti, na akiba ya fedha za kigeni ya China inazidi kuongezeka.

    Bibi Wang Chunying amesema katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia na biashara ya kimataifa imepungua. Lakini uchumi wa China umeendelea kuwa katika eneo linalofaa, na kudumisha mwelekeo wa kuendelezwa kwa madhubuti kwa ujumla. Kiasi cha ubadilishaji wa fedha za Renminbi kinatulia, mitaji inayovuka mipaka inaendelea kwa utulivu, mahitaji na utoaji katika soko la fedha za kigeni viko katika hali ya uwiano.

    Bibi Wang pia amesema katika mwaka huu mamlaka hiyo itaendelea kuhimiza kurahisisha biashara na uwekezaji wa kuvuka mipaka, kuendeleza soko la fedha za kigeni la wazi na lenye nguvu ya ushindani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako