• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa mwito wa kuwepo kwa ushirikiano kuhimiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-18 19:36:13

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa mwito wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuhimiza maendeleo ya miundombinu barani Afrika.

    Akiongea jana kwenye kongamano moja kuhusu miundombinu barani Afrika, Rais Kenyatta amesema miundombinu ya kiwango cha juu inapunguza gharama, na kuwezesha matumizi yenye ufanisi ya nguvu kazi na mitaji, na hiyo kuunganisha sehemu za uzalishaji na masoko.

    Amesema Afrika inatakiwa kufanya kazi kwa bidii kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa miundombinu yenye ufanisi.

    Rais Kenyatta amesema anaamini kuwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, wakiungwa mkono na taasisi za taifa zenye nguvu, wanahakikisha uwajibikaji na uwazi kwenye kupunguza pengo za miundombinu barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako