• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri atamani teknolojia kutangaza utalii

    (GMT+08:00) 2019-04-18 19:46:12
    Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kingwangalla, amesema Tanzania inahitaji kuwa na mpango imara wa kutumia teknolojia ya dijitali kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini vijulikane zaidi na ilivyo sasa. Alisema kitendo cha kutangaza vivutio hivyo kutasaidia kumudu ushindani mkali katika sekta hiyo kimataifa na hatimaye kupata watalii wengi zaidi na kuongeza pato la taifa.

    Waziri aliyasema haya katika ufunguzi wa kongamano la kimataifa la kuzungumzia utalii na hatima ya baadaye lililoandaliwa na Kitivo cha Utalii cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuwakutanisha wadau na wasomi katika sekta hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako