• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania : Hatua nne za kuboresha kilimo

    (GMT+08:00) 2019-04-18 19:46:33
    Spika wa Bunge Job Ndugai ametaja hatua nne za kuchukua kwa ajili ya maendeleo ya biashara zitokanazo na mazao ya kilimo na viwanda vitokanavyo na usindikaji mazao hayo. Ndugai alitoa kauli hiyo alipokuwa akifungua mhadhara wa umma kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa chakula, kukuza mnyororo wa thamani wa bidhaa zitokanazo na kilimo duniani ambao umeendeshwa na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

    Spika ametaja hatua hizo kuwa ni serikali lazima iendelee kuweka mazingira mazuriya sera ambazo zitawafanya wafanyibiashara wadogo na wa kati na viwanda vinavyosindika mazao ya kilimo kukua na kustawi. Aidha aliongeza kwa kusema kuwa wazalishaji wadogo wanahitaji msaada kuwawezesha kushindana katika soko la ndani, kikanda na kimataifa.

    Nyingine ni upatikanaji dhaifu wa huduma za fedha kwa muda mrefuzimedumaza maendeleo vijijini nchini Tanzania.

    Hatua ya nne ni uwekezaji katika utafiti wa kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako