Ndege ya kwanza aina ya Boeing 737-800NG ilipaa angani saa nne za asubuhi kutoka Kigali kwenda Kinshasa hiyo jana. Shirika hili la ndege litakuwa na safari tatu kila wiki kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kigali hadi ule wa kimataifa wa N'Djili Kinshasa, DR Congo. Safari zenyewe zitakuwa kila siku ya Jumatano, Ijumaa na Jumapili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |