• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Mtanzania mwanafunzi ashinda mbio kwa miaka miwili mfululizo nchini China

  (GMT+08:00) 2019-04-19 09:24:59

  Mtanzania Dennis Chinamo, anayesoma kozi ya uhandisi wa petroli katika chuo kikuu cha Southwest Petroleum katika Jimbo la Sichuan, mjini Chengdu China, amefanikiwa kuibuka mshindi kwenye mashindano ya mbio fupi yaliyofanyika chuoni hapo.

  Dennis alidhihirisha ubabe wake kwa mara nyingine baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika vipengele vya mbio za mita 100 na 200.

  Hii imekuwa mara ya pili mfululizo kwake kushinda michezo hiyo kwa chuo kizima, ambapo mwaka 2018 aliibuka mshindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako