• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wapinga ada ya ujenzi

    (GMT+08:00) 2019-04-19 18:38:13

    Wakenya wameonyesha ghadhabu kubwa kuhusiana na mpango wa serikali kuwatoza ada ya Mpango wa Kitaifa wa Ujenzi Nyumba, huku mahakama ikisimamisha utekelezaji wake.

    Mahakama ya Uajiri na Masuala ya Leba ilisimamisha utekelezaji huo, kufuatia kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanunuzi Bidhaa Kenya (COFEK).

    Serikali inapanga kuwatoza watu walioajiriwa asilimia 1.5 katika mishahara yao kama ada ya mpango huo.

    Jaji Maureen Onyango alitoa agizo hilo, akisema kuwa kusimamishwa kwake kutatoa nafasi ya kuunganishwa kwa kesi zilizowasilishwa na COFEK na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU).

    Ikiongozwa na Katibu Mkuu wake Stephen Mutoro, COFEK inashikilia kuwa utekelezaji wa mpango huo utawaongezea Wakenya mzigo wa ushuru mkubwa wanaotozwa na serikali.

    COFEK pia ilisema kuwa si Wakenya wote walioweka umiliki wa nyumba kama suala muhimu kwao, hivyo hawapaswi kulazimishwa kuuchangia.

    Walimu vile vile walipinga mpango huo, wakiutaja kama njama ya serikali kuendelea kuwapunja wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako