• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yateketeza kemikali za thamani ya shilingi milioni 60

    (GMT+08:00) 2019-04-19 18:39:30

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Arusha, imeteketeza zaidi ya lita 8750 za kemikali bashirifu (ethanol alcohol) zenye thamani ya Sh. milioni 60 zilizokuwa zikivushwa kuelekea nchi jirani ya Kenya bila kufuata taratibu za kisheria.

    Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Arusha, anayeshughulikia Forodha, Godfrey Kitundu, alisema kemikali hizo zilikamatwa tangu Juni 2017 na Jeshi la Polisi na ilipofika Machi 2, 2018 ilikabidhiwa kwa TRA Kituo cha Forodha cha Pamoja, (OSBP).

    Alieleza kuwa gari hilo lilikuwa na madumu ya lita 250 takribani 35 yenye kemikali hizo, ambazo ni hatari kwa jamii japo zinatumika kwa matumizi mbalimbali.

    Alifafanua kemikali hiyo hutumika kutengenezea pombe kali, manukato na hata dawa, lakini pia hutumika kutengenezea dawa haramu ya kulevya aina ya cocaine.

    Alisema baada ya kukagua na kugundua msafirishaji wa kemikali hizo hakuwa na kibali chochote, walichukua sampuli na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya vipimo zaidi.

    Aliwataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi na taratibu zake kuepusha usumbufu wa mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako