• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyibiashara wadogo kutumia siku za kutoruhusu magari kuingia jijini Kigali kukuza biashara zao

    (GMT+08:00) 2019-04-23 18:31:04
    Kundi la zaidi ya wajasiriamali 60 ambao ni wa kiwango cha chini na kati na wanaojishughulisha na kuuza bidhaa ambazo zimetengenezewa Rwanda, wamejiunga pamoja ili kuraia serikali kuu kuwapa nafasi jijini Kigali kunadi bidhaa zao. Wajasiriamali hawa wanaomba kwamba wapewe siku ambazo zimetengwa kwa magari kutoingia jijini ili kuuza bidhaa ambazo zimetengenezewa nchini humo. Sheria ya kutoruhusu magari kuingia jijini Kigali siku moja kila mwezi imekuwepo nchini Rwanda tangu mwaka wa 2015. Siku hii hutumika kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa mazoezi kando na kupunguza uchafuzi wa mazingira kutoka kwa mooashi wa magari.

    Kwa sasa, kuna mazungumzo kati ya wafanyibiashara wa binafsi na usimamizi wa jiji la Kigali kuona ni vipi siku hii itatumiwa kuinua uchumi wa Rwanda. Endapo hili litaafikiwa, basi siku hii ya kutoruhusu magari kuingia jijini Kigali, itakuwa ikitumika kunadi na kutangaza bidhaa ambazo zimetengenezewa nchini Rwanda. Watakao pewa ipao mbele ni vijana wajasiriamali wa kiwango cha chini na kati. Baadhi ya bidhaa zitakazouzwa ni sanaa,mapambo,mavazi, viatu na vinywaji vyeney asili ya Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako