• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kusaini mkopo wa shilingi bilioni 368 na China

    (GMT+08:00) 2019-04-24 20:11:20

    Kenya inatarajiwa kusaini mkopo wa shilingi bilioni 368 kutoka kwa China kwa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Naivasha hadi Kisumu. Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga wamesafiri nchini China ambako wanatarajiwa kuushawishi uongozi wa China kuwaongezea mkopo kufanikisha mradi huo.

    Ujumbe huo uliondoka Kenya jumatatu wiki hii na unajumuisha katibu katika wizara ya fedha Bw Kamau Thige, kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la reli la Kenya Bw Philip Mainga na maofisa wengine wakuu serikalini. Waziri wa uchukizi na miundo mbinu Bw James Macharia pamoja na mwenzake wa Fedha Bw Henry Rotich pia wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kusainiwa kwa mkopo huo nchini China. Awamu ya kwanza ya mradi huo unadaiwa kutumia shilingi bilioni 327 ambapo asilimia 90 ya fedha hizo ilikuwa mkopo huku Kenya ikitoa asilimia 10 pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako