• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA kuwachukulia hatua wafanyabiashara wasiotoa risiti za manunuzi

    (GMT+08:00) 2019-04-24 20:11:35

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema itamchukulia hatua za kisheria ikiwamo kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika hatoi risiti za manunuzi kwa mteja. Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani, Abdul Zuberi, katika kikao cha watumishi wa TRA na wafanyabiashara kilichofanyika jijini Mbeya. Zuberi alisema baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu kwenye biashara zao na badala yake huiibia serikali kwa kutotoa risiti za manunuzi wa wateja wao. Alisema kitendo hicho sio cha kizalendo bali kinalengo la kuiibia serikali mapato na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria. Alitoa rai kwa wafanyabiashhara kote nchini kufanya biashara zao kwa kufuata kanuni na taratibu na kuwa waaminifu katika ulipaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zitumike kwenye shughuli za maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako