• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yashauriwa kutumia taasisi za kibenki kupaa uchumi

    (GMT+08:00) 2019-04-24 20:11:56

    Tanzania imebainika ndio nchi inayotumia huduma za kibenki kwa kiwango kidogo, ukilinganisha na baadhi ya nchi zingine za Afrika Mashariki na kushauriwa kuacha kuogopa kutumia taasisi za fedha, ili waweze kuinuka kiuchumi. Ushauri huo ulitolewa na Afisa mwezeshaji kilimo fedha, kutoka Shirika la Taha, Angelina Nyansambo, ambaye alikuwa akiwajengea uwezo wakulima wa mbogamboga waliopo Halmashauri ya Babati ili waweze kubadilika na kuacha kuogopa kuzitumia taasisi za fedha.

    Alisema utafiti uliofanywa hivi karibuni kuhusu watu wa nchi za Afrika Mashariki wanavyotumia huduma za kifedha, ulibaini kuwa Tanzania inatumia huduma za kifedha kwa asilimia 17, Rwanda asilimia 21, Uganda asilimia 28 na vinara ni Kenya ambayo wananchi wake wanatumia huduma za benki kwa asilimia 40.

    Aidha, aliwataka wakulima hao kuchangamkia fursa ya kukopa katika taasisi za fedha, wakiwa tayari wameweka mipango mizuri ya kuwekeza katika kilimo biashara ili kilimo kiwe mkombozi wa maisha yao. Aliishauri serikali kushusha riba akitolea mfano kwa benki ya NMB inatoza asilimia 15, hivyo aliiomba serikali ishushe kiwango hicho ili wananchi wasiogope kukopa na wajinufaishe na fursa zilizopo kwenye taasisi za kifedha na watoke kimaisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako